• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Ufugaji

SEKTA YA MIFUGO

Idadi ya Mifugo

Mkoa wa Mbeya una jumla ya mifugo 3,095,116 kati ya hiyo idadi ya ng’ombe ni 653,304; mbuzi ni 195,569 na kondoo ni 79,850. Mchanganuo wa idadi ya mifugo ni kama inavyooneshwa katika jedwali Na. 3.4.1

Jedwali Idadi ya Mifugo kwa aina Kiwilaya hadi Juni, 2017

Mnyama 
Halmashauri
Jumla 
Busokelo 
Chunya 
Mbarali 
Mbeya (J) 
Mbeya 
Kyela 
Rungwe 
Ng’ombe (asili)

23,847

201,819

168,580

5,355

72,341

42,963

59,022

573,927

Ng’ombe (kisasa)

12,641

307

2,524

3,820

7,079

2,785

30,221

59,377

Mbuzi (asili)

9,826

33,879

85,924

4,472

33,155

4,869

21,123

193,248

Mbuzi(kisasa)

136

54

71

570

888

0

602

2,321

Kondoo

4,954

10,251

40,993

673

5,698

1,369

15,912

79,850

Nguruwe

21,982

1,646

12,843

5,096

21,646

32,887

55,213

151,313

Kuku (asili)

254,376

142,087

242,651

60,151

327,322

352,690

554,345

1,933,622

Kuku (kisasa)

8,932

0

4,273

70,323

15,000

0

2,930

101,458

JUMLA 

3,095,116 

Chanzo: Halmashauri za Wilaya na Halmashauri ya Jiji 2016

Uboreshaji wa mifugo

Mazao ya Mifugo

Mazao makuu ya mifugo yanayozalishwa ni nyama, maziwa, mayai na ngozi. Maziwa yanazalishwa kupitia wafugaji moja moja na mitandao ya ufugaji kiwilaya ukiwemo Mtandao wa wafugaji Rungwe wenye vikundi 32, MVIWAWIMBE (Halmashauri ya Mbeya) vikundi 15 na MVIWAMA (Jiji la Mbeya) wenye vikundi 11. Kuna viwanda vidogo vya kusindika maziwa ambavyo ni Mbeya Milk, Isanga Dairy Cooperative Society na MATI – Uyole vya Jijini Mbeya. Wadau wengine ni Mwasa Dairies na Faraja Group waliopo Wilayani Rungwe. Mwaka 2016/2017 lita 139,325,929 za maziwa yenye thamani ya shillingi 111,460,743,200 yalizalishwa. Aidha, Mwaka 2016/17 vipande vya ngozi 46,204 vya ng’ombe, mbuzi 31,004 na vipande 4,584 vya ngozi ya kondoo vyenye thamani ya jumla ya shilingi 231,545,600  vilikusanywa na kuuzwa ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mkoa wa Mbeya unajitosheleza katika kuzalisha nyama na kiasi kikubwa cha mifugo huuzwa nje ya Mkoa. Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 kilo 15,549,136 za nyama zilizalishwa zenye thamani ya shilingi 93,294,816,000.

Mauzo ya Mifugo na Ukusanyaji wa Maduhuli

Mkoa kwa mwaka 2016/2017 umekusanya maduhuli yenye thamani ya 36,895,750,000 baada ya kusafirisha ng’ombe 56,624 na wanyama wengine (Small Stock) 34,427. Pia  Mkoa una machinjio kubwa 33 na makaro 85 ambayo yamejengwa na kukarabatiwa kupitia miradi ya DADPs na Mpango wa Kuendeleza Ngozi Tanzania. Mkoa una majosho 77  yanayotumika. Kuna vituo 29 vya kutolea huduma za mifugo (VHS) kati ya hivyo 10 vimesajiliwa na Baraza la Veterinari Tanzania. Aidha,  Mkoa una jumla ya  maduka 720 ya kuuzia nyama. 

Katika kuepusha migororo ya wakulima na wafugaji, Mkoa kwa kupitia Halmashauri umeweza kutenga ekari 1,024,517 kwa ajili ya malisho hasa katika Halmashauri za wilaya za Chunya, Mbarali na Mbeya. Kuna shamba la kuzalisha mbegu za malisho la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi eneo la Langwila Wilayani Mbarali lenye ukubwa wa hekta 294. Shamba hili linatarajiwa kuzalisha mbegu za malisho kwa ajili ya mashamba darasa ya malisho na mashamba ya malisho ya taasisi  na watu binafsi. Pia Kituo cha Utafiti wa Mifugo – Uyole huzalisha na kusambaza mbegu aina ya Rhodes Boma, miti malisho na majani makavu (Hay) kwa  ajili kituo na wafugaji.

Katika kutekeleza agizo la Mheshimiwa Makamu wa Rais la kutambua na kusajili mifugo nchini,Mkoa kupitia Halmashauri umekamilisha kazi ya kuwatambua na kuasajili wafugaji na mifugo. Kazi ya kupiga chapa na kuweka heleni ng’ombe wa asili 573,927 na wa maziwa 59,377 umezinduliwa rasmi na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa katika Halmashauri za Chunya tarehe 11.07.2017 na Mbarali tarehe 14.07.2017. Zoezi la kupiga chapa na kuweka heleni linatajia kukamilika ifikapo tarehe 31.07.2017

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Matokeo ya Kidato cha Sita 2020 August 21, 2020
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021 Mkoa wa Mbeya. December 18, 2020
  • Fomu za Maelekezo kwa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano 2021 Shule za Mkoa wa Mbeya (Joining Instructions) June 07, 2021
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • RC Homera atoa siku 14 Tarura kupata Mkandarasi Mpya

    February 23, 2023
  • WAZIRI DKT MABULA AZINDUA MPANGO KABAMBE WA JIJI LA MBEYA

    February 21, 2023
  • WATOTO 5,236 WAPANGIWA VYUO MBALIMBALI VYA UFUNDI MKOANI MBEYA

    February 06, 2023
  • "Wananchi Tushirikiane kutokomeza ukatili wa Kijinsia" Rc Homera

    December 02, 2022
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025 2503034

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa