• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Waziri Mkuu Mstaafu Mh Pinda Afunga Maonesho ya Nanenane Mbeya

Imetumwa : August 8th, 2019

Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne, Mizengo Pinda amewashtua viongozi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na viongozi wengine wa wilaya  alipowaambia mikoa yao ni miongoni mwa mikoa 10 inayoongoza kwa utapiamlo wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini.

Pinda ametoa kauli hiyo leo Agosti 8, wakati akifunga maonyesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi wa mikoa hiyo yaliyofanyikakwenye uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya.

Amesema kitaifa asilimia 33 ya watoto 100 wanautapiamlo, lakini  mkoa wa Ruvuma  una asilimia 40 yawatoto 100 wenye utapiamlo , wakati mkoa wa Iringa una asilimia 47.1 , Mbeya asilimia 33.8, na Mkoa wa Rukwa ni asilimia 47.9.

Mikoa mingine ni Njombe ambao una asilimia 53,mkoa wa Katavi una asilimia 33.7 na Mkoa wa Songwe una asilimia 43.3 idadi ambayo alisema ni kubwa na inatia aibu kwa mikoa inayotajwa kuongoza kuzalisha chakula.

Mwaka 2018 mikoa hiyo yenye watu zaidi ya watu milioni nane ilizalisha kwa asilimia 124 ya malengo na hivyo kuwa na ziada yatani milioni 3.2 ya chakula .

Pinda ambaye anajulikana kwa jina la mtoto wa mkulima amesema tatizo hilo ni la hovyo na kuwataka wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kuanzisha mkakati maalumu wa kupambana na utapiamlo kwa watoto haona wajawazito ili kuondoka na  aibu.

Amesema jambo hilo limemfanya yeye kwa kushirikiana na wadau kuanzisha taasisi itakayofanya kazi ya kupambana na utapiamlo nchini hususan mikoa inayoongoza kwa tatizo hilo.

Ameitaka mikoa yote kushirikiana na na vyuo mbalimbali kutatua changamoto za jamii hususan suala la kutoa elimu kuhusu lishe bora.

Akizungumzia ujasiriamali wake kwa ufugaji wa samaki alisema  yeye anamiliki mabwawa tisa Dodoma yaliyochimbwa kwa gharama ya sh 3.5 milioni  na kuweka samaki ambao akivuna bwawa moja linampatia Sh 25 milioni baada ya miezi  michache.

Ametoa mwito kwa vijna kufanya ujasiriamali  kwa guvu zote bila kusubiri ajira ambazo kwa kawaida siyo nyingi katika nchi zote duniani.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert  Chalamila , amesema wakuu wa mikoa waliamua kumwalika yeye kufunga maonyesho hayo  baada ya kuvutiwa na uadilifu wake  na kwamba Pinda ni kiongozi mwadilifu wa kuigwa na viongozi wasasa.

Mhe. Chalamila amekemea viongozi wanaoendekeza rushwa na uzembe katika Serikali ya awamu ya Tano na kwamba hawana budi kuacha mara moja badala yake watekeleze maagizo na maelekezo ya Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Matokeo ya Kidato cha Sita 2020 August 21, 2020
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021 Mkoa wa Mbeya. December 18, 2020
  • Fomu za Maelekezo kwa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano 2021 Shule za Mkoa wa Mbeya (Joining Instructions) June 07, 2021
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • RC Homera atoa siku 14 Tarura kupata Mkandarasi Mpya

    February 23, 2023
  • WAZIRI DKT MABULA AZINDUA MPANGO KABAMBE WA JIJI LA MBEYA

    February 21, 2023
  • WATOTO 5,236 WAPANGIWA VYUO MBALIMBALI VYA UFUNDI MKOANI MBEYA

    February 06, 2023
  • "Wananchi Tushirikiane kutokomeza ukatili wa Kijinsia" Rc Homera

    December 02, 2022
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025 2503034

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa