• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Wafanyakazi waaswa kuepuka Malumbano ya Kisiasa

Imetumwa : September 3rd, 2018

Watumishi wa Umma watakiwa kutokuwa sehemu ya ushabiki wa kisiasa  na kupotosha jamii bali wawe mabalozi wazuri wa kutafsiri agenda za serikali katika kutekeleza dhana ya uwajibikaji katika kuleta maendeleo ya taifa na mkoa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na leo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila wakati akiongea na watumishi wa umma Wilaya ya Mbarali na kusema Serikali haitawavumilia watumishi wanaoingiza itikadi za vyama kwenye utumishi wa umma.

Mhe Chalamila  amesema kuwa mtumishi wa umma anaongozwa na kanuni, sheria na taratibu ambavyo vimemnyang’anya uwezo wa kuipinga serikali badala yake kuwa mshauri wa serikali katika shughuli za maendeleo.

“ Ni aibu kuona mtumishi wa umma anabadili uelekeo na kuwa mpinzani wa serikali kwa kuwapotosha wananchi na sitasita kumchulia hatua mtumishi huyo kwa mujibu wa sheria na taratibu za utumishi wa umma.” Mhe Chalamila

Chalamila amesema wataalamu wakiwa na agenda ya kuipinga serikali wanatakiwa kutoka katika sehemu ya serikali na kuwa wanasiasa ili kuendeleea kuipinga serikali katika majukwaa ya siasa.

Amewataka watumishi kusoma kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili ziweze kuwaongoza katika utendaji kazi wao ili kuepuka mihemko ya kisiasa ambayo inaweza kusababisha migongano ya kimaslahi ya kiutendaji katika maeneo yao ya kazi,

Aidha, Mhe Chalamila amewataka watumishi wa taasisi za umma waliopewa mamlaka kutokuwa chanzo cha kuleta malalamiko au chombo cha kuwatisha wananchi kwa kuendelea kusimamia sheria na taratibu za serikali kwa kuwa waadilifu.

“Mnatakiwa kutoa huduma kwenye taasisi zenu kwa kuangalia sera na agenda ya nchi sasa ikiwa ni kuwahudumia wananchi kwa uadilifu ili kujenga uaminifu kwa wananchi mnao wahudumia” Mhe Chalamila.

Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bibi Mariam Mtunguja amewataka watumishi wa umma kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuwahudumia awananchi kwa taratibu, sheria na haki.

Bibi Mtunguja amesema kuwa wataalamu wa kiutendaji ndio wasaidizi wakuu wa Mkuu wa Mkoa katika kutekeleza majukumu ya maendeleo katika mkoa na hivyo ni muhimu kuwa na ushirikiano wa karibu katika utendaji kazi.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Matokeo ya Kidato cha Sita 2020 August 21, 2020
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021 Mkoa wa Mbeya. December 18, 2020
  • Fomu za Maelekezo kwa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano 2021 Shule za Mkoa wa Mbeya (Joining Instructions) June 07, 2021
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • RC Homera atoa siku 14 Tarura kupata Mkandarasi Mpya

    February 23, 2023
  • WAZIRI DKT MABULA AZINDUA MPANGO KABAMBE WA JIJI LA MBEYA

    February 21, 2023
  • WATOTO 5,236 WAPANGIWA VYUO MBALIMBALI VYA UFUNDI MKOANI MBEYA

    February 06, 2023
  • "Wananchi Tushirikiane kutokomeza ukatili wa Kijinsia" Rc Homera

    December 02, 2022
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025 2503034

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa