Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Zuberi Homera ametoa siku 14 kwa Wakala wa barabara za mijini na vijijini (Tarura) kuhakikisha anapatikana mkandarasi wa kukamilisha ujenzi wa barabara yenye urefu kilometa 1.5 iliyotekelezwa na mkandarasi wa kampuni ya Canopies International (T) Limited baada ya kusitishiwa mkataba wake.
Homera aliyasema hayo siku ya Alhamisi Februari 23, 2023 mara baada ya kufanya ziara ya kukagua barabara hiyo inayounganisha Vijiji vya Lupeta, Izumbwe na Wimba huku ikiwa kiungo kwa usafirishaji wa mazao ya chakula na biashara hususani viazi mviringo na mboga mboga.
"Nimepigiwa simu na wananchi wanahangaika sana juu ya kusafirisha mazao kutokana na kwakusuasua kwa utekelezaji wa mkandarasi aliyepewa tenda licha ya kulipwa asilimia 70 ya kazi yake"alisema.
Uzunguni Road
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025 2503034
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa