• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Maji
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Prof Mkenda Azindua Programu ya AGRI CONNECT

Imetumwa : June 21st, 2021

Shabaha ya serikali ni kuhakikisha utafiti wa mbegu bora unaimarishwa, kuongeza uzalishaji wa mbegu lakini pia kuboresha utoaji wa huduma za ugani maeneo mengine yatakayoangaliwa ni pamoja na kilimo cha umwagiliaji hususani katika uzalishaji wa mbegu ili kuweza kujitosheleza kwa mbegu mwaka mzima; kuimarisha upatikanaji wa suluhu katika masoko ya mazao ya kilimo; kuimarisha Kilimo Anga ili kudhibiti visumbufu vihamavyo pamoja na kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa mitaji na ugharamiaji wa sekta ya kilimo.

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo tarehe 21 Juni 2021 kwenye uzinduzi wa Programu ya AGRI CONNECT uliofanyika Jijini Mbeya

Itakumbukwa kuwa Mwaka 2018, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango ilisaini Mkataba wa Ugharamiaji (Financing Agreement) na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya wa utekelezaji wa Programu ya AGRI-CONNECT wenye thamani ya Euro milioni 100 sawa na takribani Shilingi bilioni 277 ambazo ni ruzuku (grant) kutoka Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.

Aidha, kiasi cha Euro milioni 3.5 sawa na Shilingi bilioni 9.6 zimechangiwa na wadau wanaotekeleza programu hii ya AGRI-CONNECT na kufanya mahitaji ya rasilimali kuwa Euro milioni 103.5 sawa takribani bilioni 287 kwa kipindi cha miaka miaka minne kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2023/2024 ambapo utekelezaji wake ulianza Februari, 2019 kwa hatua za awali.

AGRI-CONNECT imechagua maeneo machache ya kipaumbele yenye kugusa watu wengi kwa kuzingatia mnyororo wa thamani (agricultural value chain) wa mazao ya kahawa, chai na mazao ya Bustani ambapo wakulima wadogo wapatao 150,000 wa mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe, Katavi, Iringa na Ruvuma watanufaika.

Waziri Mkenda ameitaka AGRI-CONNECT ijikite katika kuongeza uzalishaji na tija kwenye mazao haya iliojiwekea kuwa ni ya kipaumbele na kutafuta suluhu ya tatizo la masoko. Kama itatekeleza vizuri AGRI-CONNECT, kuwa uzalishaji wa mazao utaongezeka.

Kuhusu ujenzi wa miundombinu, hususani ya usafiri. Waziri Mkenda ameutaka Wakala wa Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara Vijijini (TARURA) kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara za vijijini hususani barabara zinazounganisha maeneo ya uzalishaji na masoko.

Kadhalika Waziri Mkenda ametoa mwito kwa sekta binafsi kuhakikisha AGRI-CONNECT inatekelezwa. “Serikali ni lazima ishirikiane na Sekta binafsi. Hivyo basi, mamlaka zote za mikoa ya nyanda za juu kusini na Mamlaka zingine zote husika zishirikiane na Sekta binafsi kwenye mnyororo wa thamani wa mazao yote ya kilimo hususan Kahawa, Chai na mazao ya bustani. Katika mazao haya kuna fursa nyingi ambazo sekta binafsi inaweza kunufaika nazo, ikiwa ni pamoja na kujenga viwanda” Amekaririwa Prof Mkenda

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera amesema kuwa mradi huo wa AGRI CONNECT unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya ni muhimu hapa nchini kwani itakuwa sehemu ya kupambana na utapiamlo na udumavu ambao kiwango chake ni kikubwa.

“Kiwango cha udumavu na utapiamlo ni kikubwa sana hapa nchini ambapo mkoa wa Ruvuma ni asilimia 41%, Iringa 47.1%, Mbeya 33.8%, Njombe 53.6%, Songwe 43.3% na Katavi 73.7% hivyo tunaamini mradi huu utamaliza kama sio kupunguza tatizo hilo” Amesisitiza Rc Homera

Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe Omary Mgumba amesema kuwa Mkoa wa Songwe unashika nafasi ya tatu kwa kilimo cha kahawa nafasi ya tatu katika uzalishaji wa mazao ya chakula.

Amesema pia pamoja na kushika nafasi hizo nzuri za kiuongozi katika sekta ya chakula lakini bado mkoa huo upo katika nafasi mbaya kwa kuongoza kwa wananchi kuwa na utapiamlo pamoja na udumavu.

“Hivyo mradi huu unakuja kuwasaidia wakulima wenzangu hususani wa kahawa kwani jinsi mpango ulivyo utaimarisha sekta mbalimbali ikiwemo barabara kwa ajili ya kuboresha urahisi wa kuyafikia masoko ya mazao ya wakulima” Amekaririwa Mhe Mgumba

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Dkt. Christine Ishengoma (Mb) amesema kuwa mradi huo utakaotengeneza barabara za vijijini utarahisisha usafirishaji wa mazao ya wakulima nchini.

Amesema kuwa ni matarajio makubwa kwa bunge na serikali kwa ajira zitakazotolewa kwa vijana na kina mama kwa ajili ya kujikimu katika mahitaji yao katika familia zao.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera amesema kuwa mradi huo wa AGRI CONNECT unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya ni muhimu hapa nchini kwani itakuwa sehemu ya kupambana na utapiamlo na udumavu ambao kiwango chake ni kikubwa.

Matangazo

  • Fomu za Maelekezo kwa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano 2021 Shule za Mkoa wa Mbeya (Joining Instructions) June 07, 2021
  • Matokeo ya Kidato cha Sita 2020 August 21, 2020
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021 Mkoa wa Mbeya. December 18, 2020
  • Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji March 11, 2021
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • "Wananchi Tushirikiane kutokomeza ukatili wa Kijinsia" Rc Homera

    December 02, 2022
  • Wakuu wa Wilaya Mbeya wasaini Mkataba wa Afua za Lishe

    October 11, 2022
  • RC HOMERA AWATAKA ASKARI WA BARABARANI KUWACHUKULIA HATUA MADEREVA WANAOKIUKA SHERIA.

    September 15, 2022
  • Mbeya Vinara Mchezo wa Mpira wa Miguu UMISETA NA UMITASHUMTA

    August 24, 2022
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025 2503034

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2019 Mbeya Region . All rights reserved.