• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Apokea Vyumba vya Madarasa kutoka Bioland

Imetumwa : February 14th, 2018

MKUU wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla amepokea vyumba viwili vya madarasa na kimoja cha Ofisi ya walimu vilivyojengwa kwa msaada mkubwa wa Kampuni inayojishughulisha na unuzuzi wa zao la Kakao wilayani Kyela ya Kim’s chocolate(Belgium) Bioland International katika Shule ya msingi Ngana iliyopo wilayani hapa.

Mhe Makalla pia amepokea madarasa vyumba viwili vya madarasa vilivyojengwa na Kampuni hiyo katika Shule ya Msingi Lubele iliyopo katika kata ya Ikimba.

Kwa mujibu wa Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela,Mwalimu Polemone Ndarugiliye ujenzi wa vyumba vitatu katika shule ya msingi Ngana ulioambatana na ukarabati wa vyumba vingine viwili shuleni hapo uligharimu Shilingi 23,271,000 ambapo kampuni ya Bioland ilichangia Shilingi 17,000,000 sawa na asilimia 73.1,wananchi Shilingi 5,128,000 sawa na asilimia 22 kupitia nguvu kazi.

Mwalimu Ndarugiliye amesema Serikali kupitia fedha za mfuko wa jimbo ilichangia shilingi 600,000 sawa na asilimia 2.6 na Shule ya Msingi Ngana kupitia fedha za ruzuku ikachangia Shilingi 534,000 sawa na asilimia 2.3.

Amesema kwa Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya msingi Lubele uliogharimu Jumla ya Shilingi 14,756,500 mchango wa Kampuni hiyo ni Shilingi 9,821,000,wananchi kupitia nguvu kazi Shilingi 4,352,000,Diwani Shilingi 682,000 na madhehebu mbalimbali ya dini Shilingi 201,000.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo,Makalla aliwataka wakazi wilayani hapa kuendelea kushirikiana kwa karibu na Kampuni hiyo kwakuwa inaonyesha jitihada nzuri za kuboresha miundombinu ya Elimu.

Kwa upande wake Afisa kutoka Kampuni ya Bioland,Fons Maex amesema kampuni bado ina utayari wa kuendelea kusaidia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu katika Shule zote za msingi zilizopo kwenye Halmashauri za Kyela,Rungwe na Busokelo.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Matokeo ya Kidato cha Sita 2020 August 21, 2020
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021 Mkoa wa Mbeya. December 18, 2020
  • Fomu za Maelekezo kwa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano 2021 Shule za Mkoa wa Mbeya (Joining Instructions) June 07, 2021
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • RC Homera atoa siku 14 Tarura kupata Mkandarasi Mpya

    February 23, 2023
  • WAZIRI DKT MABULA AZINDUA MPANGO KABAMBE WA JIJI LA MBEYA

    February 21, 2023
  • WATOTO 5,236 WAPANGIWA VYUO MBALIMBALI VYA UFUNDI MKOANI MBEYA

    February 06, 2023
  • "Wananchi Tushirikiane kutokomeza ukatili wa Kijinsia" Rc Homera

    December 02, 2022
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025 2503034

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa