• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Maji
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mbeya Super Cup 2021 Yahitimishwa

Imetumwa : August 25th, 2021

Mashindano ya Mbeya Super Cup yaliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Zuberi Homera tarehe 19/08/2021 hatimaye yamefika tamati tarehe 25/8/2021. Mashindano hayo yameweza kuhusisha timu kutoka halmashauri zote za Mbeya ambazo ni Halmashauri ya Rungwe, Halmashauri ya Kyela, Halmashauri ya Chunya, Halmashauri ya Busokelo, Halmashauri ya Mbarali na Halmashauri ya jiji la Mbeya. Mashindano hayo yalikuwa na lengo la kutafuta vipaji kwa Mkoa wa Mbeya ili kuweza kuzipa usajili timu za ligi kuu na daraja la kwanza zikiwepo Prison fc, Mbeya city fc, Mbeya kwanza na nyinginezo na kuunda timu ya mkoa kutokana na mashindano hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mheshimiwa Juma Zuberi Homera amemshukuru mheshimiwa Rais  wa Jamuhuri ya Muungano  wa Tanzania mama Samia suluhu Hassan kwa kuweza kuendeleza michezo nchini ili kuweza kukuza vipaji kwa vijana, na pia amemshukuru Mbunge wa jiji la mbeya Dr Tulia Aksoni na wabunge wengine kwa kutoa jezi kwa timu ambazo zinatoka katika majimbo yao na viongozi wa wilaya zote za Mbeya na Mstahiki Meya mheshimiwa Dormohamed Issa Harmat na Mkurugenzi wa jiji l Mbeya  kwa kushiriki na kukubali  mashindano hayo yafanyike katika jiji la Mbeya.

Mheshimiwa Juma Zuberi Homera ametoa hamasa kwa vijana mbalimbali kuwa mashindano haya ni endelevu kwa kila mwaka kwa lengo la kuwapa fulsa vijana kuonesha vipaji vyao katika ligi kuu au madaraja ya chini maana inawapa vijana hali ya kupambana ili kufikia malengo, amesema hayo baada ya kuwakabidhi kombe washindi wa mashindano hayo timu ya uyole Worriors baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Kyela Combine kwa goli moja kwa sifuri.

Aidha Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya  Bi. Anjelina hakusita kuishukuru kamati ya mashindano ya Mbeya Super Cup ambayo yalisimamiwa na Mkurugenzi wa jiji la Mbeya mheshimiwa Amede Ng’wanidako pamoja na Meya wa jiji la Mbeya mheshimiwa Dormohamed Issa Rahmat ambao wameweza kuiongoza kamati nzima ya mashindano na kuweza kufikia tamati  tarehe 25/8/2021 na pia Mheshimiwa Bi. Anjelina amewashukuru wadhamini wote kwa kudhamini mashindano haya na kuwashukuru wanahabari wote ambao waliweza kushiriki katika kutangaza na kusambaza taarifa za mashindano hayo ambayo bila wao wasingepata pongezi kwa Halmashauri nyingine

Mashindano hayo yaliweza kutamatika hapo tarehe 25/08/2021 kwa kuweza kuhusisha timu nane za kutoka Halmashauri zote za Mbeya na kupata mshindi kutoka Halmashauli ya mbeya jiji la Mbeya kwa timu ya Uyole Worriors na kufanikiwa kuchukua kombe lenye thamani ya 500,000/= na fedha tasilimu 5,000,000/= na mshindi wa pili Kyela combine wamepata fedha taslimu 3,000,000/= na mshindi wa tatu Mbeya Dc wamepata fedha taslmu 2,000,000/=

Mashindano hayo yameweza kuibua vipaji vya wachezaji thelathini na sita na pia Mkuu wa Mkoa amesema watakaa kambini na kufanya mchujo tena na kutafuta wachezaji ishirini na tano kwa lengo la kupata timu iliyokamilika kama timu ya mkoa. Mashindano hayo yatafanyika kila mwaka na kwa mwaka utaofuata kila wilaya itafanya mashindao ya wilaya kujumuisha Kata zao na kutoa timu ambazo zitajumuika katika mashindano ya Halmashauri zote na kutoa  timu ya Mkoa wa Mbeya.

Matangazo

  • Fomu za Maelekezo kwa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano 2021 Shule za Mkoa wa Mbeya (Joining Instructions) June 07, 2021
  • Matokeo ya Kidato cha Sita 2020 August 21, 2020
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021 Mkoa wa Mbeya. December 18, 2020
  • Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji March 11, 2021
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • "Wananchi Tushirikiane kutokomeza ukatili wa Kijinsia" Rc Homera

    December 02, 2022
  • Wakuu wa Wilaya Mbeya wasaini Mkataba wa Afua za Lishe

    October 11, 2022
  • RC HOMERA AWATAKA ASKARI WA BARABARANI KUWACHUKULIA HATUA MADEREVA WANAOKIUKA SHERIA.

    September 15, 2022
  • Mbeya Vinara Mchezo wa Mpira wa Miguu UMISETA NA UMITASHUMTA

    August 24, 2022
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025 2503034

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2019 Mbeya Region . All rights reserved.