• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
        • Orodha Mpya ya Vitu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Katibu Tawala Mkoa Azindua Mafunzo ya PlanRep Mbeya

Imetumwa : August 7th, 2017

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bibi Mariam Mtunguja amezitaka Halmashauri zote ambazo hazijaingia wala kupata mafunzo kutoka kwenye Mpango wa Uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma(PS3) kuhakikisha zinatenga bajeti ili kuingia kwenye mfumo huo.

Bibi Mtunguja ametoa wito huo leo alipokuwa anafungua mafunzo ya Mfumo mpya wa kuandaa mipango na bajeti za Mamlaka ya Serikali za mitaa (PlanRep) na kuimarisha utoaji huduma kwa Wananchi nchini yaliyofanyika katika ukumbi wa Usungilo Jijini Mbeya.

Amesema kuwa kupitia mfumo huo ambao umeboreshwa unakwenda kuondoa changamoto ambazo zilikuwepo  kwenye mfumo wa zamani hivyo ni muhimu kwa kila Halmashauri nchini kupata mafunzo haya.

Bibi Mtunguja amesema kuwa kutokana na mabadiliko  haya na kurahisishwa kwa teknolojia  mfumo mpya wa PlanRep umerahisishwa  kwa kufanywa  kuwa "Web Based" na utawezesha Halmashauri kuingiza  taarifa za mipango na bajeti moja kwa moja kwa njia ya mtandao na kutumwa kwenye mfumo  uliopo OR- TAMISEMI.

Naye Mwakilishi wa Mradi wa PS3 Dr. Gemin Mtei amesema kwamba mradi huo unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani (USAID) ulipelekwa kwenye mikoa 13 na Halmashauri 93 za Tanzania bara ambapo mfumo huu ni wa Kitaifa na uko kwenye toleo la mfumo wa Kielektroniki ambao unatambulisha teknolojia ya mawasiliano na kufanya upatikanaji wake kuwa rahisi mahali popote na muda wowote.

Dr. Mtei amesema kuwa mafunzo hayo yanatolewa na timu ya Wakufunzi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa,Wakala wa Serikali Mtandao(eGA) Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Fedha na Mipango,PS3  pamoja na Wizara ya Afya.

 Mafunzo hayo yamehudhuriwa na  Maafisa Mipango, Wahasibu, Wachumi, Maafisa Tehama na Makatibu wa Afya wa Halmashauri zote kutoka Mikoa minne ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.



Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU "MOCK" KIDATO CHA NNE MKOA WA MBEYA 2024 August 20, 2024
  • FOMU YA MAOMBI YA USHIRIKI WA MAONESHO YA NANENANE 2024 July 23, 2024
  • Fomu ya Maombi Ushiriki wa Maonesho ya Nanenane_2023-_Kiswahili July 03, 2023
  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA SHEREHE ZA NANE NANE NYANDA ZA JUU KUSINI YAANZA KWA KISHINDO

    April 30, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA IMES

    April 29, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YARIDHISHWA NA MAJIBU YA WADAU KUHUSU MAPENDEKEZO UGAWAJI WA JIMBO LA MBEYA MJINI.

    April 25, 2025
  • DKT. HOMERA AAGIZA MRADI KUKAMILIKA HARAKA IWEZEKANAVYO ILI WANANCHI WAPATE HUDUMA

    April 14, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • EOFFICE
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiria Nje ya Nchi
  • Tovuti ya Serikali

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025-2504045

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa