• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Uwekezaji, Viwanda na Biashara
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Tehama na Takwimu
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri za Vijiji Zatakiwa Kuwa na Mpango Bora wa Ardhi

Imetumwa : March 8th, 2020

Hayo yamesemwa na mjumbe  wa Kamati Maalumu ya Uelimishaji Wananchi Juu ya Umuhimu wa Uhifadhi na Ujirani Mwema, Afisa Mipango Miji Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndg. Enock Kyando alipokuwa akiwasilisha mada yake ya matumizi bora ya Ardhi katika vijiji vya Uturo, Mtamba, Ukwama na Kapunga Wilaya ya Mbarali siku ya tarehe 07/03/2020.

Kyando alisema kuwa wanakijiji wanapaswa kuzisimamia Serikali zao za kijiji ili ardhi yao isichukuliwe bila kufuata utaratibu kwani kuna baadhi ya sehemu baadhi ya viongozi wamekuwa sio waaminifu wanagawa ardhi ya kijiji bila kuwashirikisha wenye ardhi yao.

*“Msimamizi mkuu wa ardhi ya Kijiji ni Serikali ya kijiji kupitia mkutano mkuu, mtu yeyote anaehitaji kumiliki ardhi ya kijiji anatakiwa kupitishwa kwenye mkutano mkuu ili apangiwe matumizi ya ardhi aliyoiomba, Mtendaji na Mwenyekiti kazi yao ni kupokea maombi tu, Ardhi ni kitu cha muhimu, tusipoisimamia vizuri tutakuja kupigana wenyewe kwa wenyewe”* alisema Kyando

Kyando aliongeza kuwa kijiji kinatakiwa kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi kwani itaondoa migogoro ya mipaka mbalimbali vilevile ni chombo kinachoonesha ni kiasi gani cha ardhi kilichopo kwa ajili ya shughuli za kijiji kama mifugo, kilimo, makazi, viwanda pamoja na matumizi mengine.

Aliongeza kuwa sambamba na kuwa na matumizi bora ya ardhi ya kijiji ni vizuri kila mtu mwenye kipande cha ardhi akachukua hati yake ya kimila yake  ambayo inapatikana ofisi ya kijiji ili awe amemiliki kisheria kwani Hati  miliki ya kimila ina hadhi sawa na hati miliki zingine za ardhi.

Aidha, Mjumbe mwingine wa timu ya uelimishaji Afisa Mipango Miji Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg Geofrey Mwaijobele amesema kuwa ardhi haiongezeki bali wanadamu na mifugo ndio vinaongezeka kwa kasi hivyo ni muhimu Serikali za vijiji kuweka kipaumbele mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji.

Mwaijobele ameongeza kuwa kama maeneo ya misitu na malisho ya mifugo yamehifadhiwa na kijiji ni vyema kila mwananchi akahusika kuyalinda maeneo hayo.


Baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye mikutano hiyo wameishukuru timu ya uelimishaji iliyoundwa kwani wameongeza uelewa wa masuala ya uhifadhi, kwani walikuwa wanavunja sheria bila kujiua na kupitia elimu hiyo watawaelimisha na wengine ili kudumisha ujirani mwema na wahifadhi.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOPANGWA KATIKA VITUO VYA UFUNDI STADI NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI MKOA WA MBEYA February 03, 2023
  • Matokeo ya Kidato cha Sita 2020 August 21, 2020
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021 Mkoa wa Mbeya. December 18, 2020
  • Fomu za Maelekezo kwa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Tano 2021 Shule za Mkoa wa Mbeya (Joining Instructions) June 07, 2021
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • RC Homera atoa siku 14 Tarura kupata Mkandarasi Mpya

    February 23, 2023
  • WAZIRI DKT MABULA AZINDUA MPANGO KABAMBE WA JIJI LA MBEYA

    February 21, 2023
  • WATOTO 5,236 WAPANGIWA VYUO MBALIMBALI VYA UFUNDI MKOANI MBEYA

    February 06, 2023
  • "Wananchi Tushirikiane kutokomeza ukatili wa Kijinsia" Rc Homera

    December 02, 2022
  • Tazama Zaidi

Video

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA MBEYA
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko
  • Mafanikio ya TASAF
  • OPRAS Fomu
  • Fomu ya Matibabu

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025 2503034

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa