• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Maji
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Watumishi watakiwa Kuelewa Misingi ya Utumishi wa Umma

Imetumwa : September 10th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila amewataka watumishi wa umma  halmashuri ya Kyela kuelewa misingi ya utumishi wa umma na kuacha  mihemko ya kisiasa na kushindwa kuwahudumia wananchi.

Mhe.Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea na watumishi mbalimbali wa halmashauri na taasisi za umma kwenye ziara ya kujitambulisha na kusema kuwa hakuna demokrasia isiyo dhibitiwa na sheria na kanuni

Mhe Chalamila amewataka watumishi wa umma kuwa waadilifu na kutumia vizuri mamlaka waliopewa na kutokuwa chanzo cha kuongeza malalamiko ya wananchi kwa Serikali bali wametakiwa kutoa huduma bora kwa kuangalia sera na agenda ya nchi kwa sasa.

Amewataka Maafisa mipango na biashara kujitafakari wanaisaidia vipi halmashauri yao na kuagiza wataalamu hao kuwa wabunifu kwa kuandika maandiko ya kutengeneza vitega uchumi vinavyoweza kusaidia na kuiongezea halmashauri mapato ya ndani katika sekta za afya, elimu, viwanda na utalii.

Katibu Tawala wa Mkoa Bibi Mariam Mtunguja amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa ushirikiano na kusema kuwa wataalamu wa kiutendaji ndio wasaidizi wakuu wa Mkuu wa Mkoa katika kutekeleza majukumu ya maendeleo katika mkoa na hivyo ni muhimu kuwa na ushirikiano wa karibu katika utendaji kazi.

Aidha, Mhe Mkuu wa Mkoa amepata fursa ya kutembelea kituo cha forodha katika Mamlaka ya Mji Mdogo Kasumulu na kukitaka kituo hicho kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato na kusema jambo hili linawezekana kama taasisi zote zitafanya kazi kwa pamoja ili kubadilishana ujuzi katika maeneo yao.

Ameitaka mamlaka ya forodha kukaribisha mawazo tofauti ya jinsi ya kutanua uwezo wa ukusanyaji wa mapato kwa kushirikisha mawazo mapya kutoka kwenye mamlaka nyingine ikiwa pamoja na wananchi wa eneo husika.

Mhe Chalamila ameitaka mamlaka hiyo pia kusimamia ulinzi na usalama wa mpaka kwa kuimarisha ulinzi na watu wajue kuwa mpaka unalindwa  kwani eneo hilo ni rahisi kupitika kwa wahamiaji haramu na magengo.

“kuna baadhi ya watumishi sio waadilifu katika kusimamia ulinzi wa mipaka lakini na walio waadilifu wanaitwa “wanoko”. Ni bora kuitwa “mnoko” kwa kusimamia sheria na kanuni za nchi kuliko kupendwa kwa kuvunja sheria na taratibu za Serikali” alifafanua Mkuu wa Mkoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ulrich Matei  amewataka watumishi wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa kushirikiana kwa sababu mpaka huo umekuwa ukitumika sana kwa njia za panya kupitishia magendo, dawa za kulevya pamoja na wahamiaji haramu.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi Matei amewataka pia kuangalia ulinzi na usalama wa bidhaa zinazotoka na kuingia katika mpaka huo ili kujua madhara yake na kuhakikisha wanafunga njia zote za panya zinazotumiwa na wafanyabiashara kupitisha magendo hayo.  

Matangazo

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2018 January 24, 2019
  • Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2019 Mkoa wa Mbeya. December 17, 2018
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • Maafisa Upelelezi Watakiwa Kufanya Kazi kwa Weledi

    February 01, 2019
  • Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Atoa Msaada wa Mabati

    January 09, 2019
  • GSM Yakabidhi Mifuko 140 kwa RC Mbeya

    November 30, 2018
  • TBS Watakiwa Kufanya Kazi kwa Ushirikiano

    November 12, 2018
  • Tazama Zaidi

Video

Viongozi watakiwa kuwa wasafi
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Bajeti ya Mkoa wa Mbeya 2018/2019
  • Mpango wa Bajeti 2018/2019
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Fomu ya Ruhusa
  • OPRAS Fomu
  • Maoni na Malalamiko
  • Mwongozo Uwekezaji Mkoa wa Mbeya
  • Mafanikio ya TASAF

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 022 253034

    Simu ya Mkononi: 255 784838650

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Haki Miliki@ 2018 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa