• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mbeya Region
Mbeya Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mbeya

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu
      • Maji
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Menejimenti ya Serikali za mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Mbeya
    • Chunya
    • Mbarali
    • Rungwe
    • Kyela
  • Halmashauri
    • Kyela
    • Busokelo
    • Mbeya
    • Chunya
    • Rungwe
    • Mbarali
    • Jiji la Mbeya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Ziwa Ngozi
      • Milima ya Mbeya
      • Daraja la Mungu
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Maji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Nyaraka
    • Sheria
    • Fomu ya Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mhe Rais Magufuli Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Maktaba MUST

Imetumwa : May 3rd, 2019



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuliameutaka uongozi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kutumia wakandarasi ndani wanaosoma katika chuo hicho katika ujenzi wa majengo ya mabweni na maktaba ili yakamilike kwa wakati.

Mhe. Rais Magufuli ameyasema leo katika sherehe za uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa maktaba na kuwapongeza Viongozi wa MUST kwa lengo la kupanua udahili wa wanafunzi kutoka 4630 wa sasa hadi kufikia 15000 ifikapo  2025.

Mhe.Rais Magufuli  ameahidi kutoa shilingi bilioni 2.9 na kuwataka viongozi wa chuo kutumia wakandarasi ambao wamekuwa wakitumika kujenga majengo mbalimbali ya Serikali ikiwemo shule kongwe 15, vyuo  vya maendeleo ya wananchi 18, hospitali na majengo ya wizara Mkoani Dodoma.

Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali itahakikisha chuo hicho kinaimarishwa ili kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Hayati Mwl  Julius Kambarage Nyerere aliyetaka Taifa liwe na chuo imara cha Sayansi na Teknolojia na kutokana na dhamira hiyo Serikali itatoa  shilingi 5 bilioni kwaajili ya Ujenzi wa mabweni ya wanafunzi,  na kuiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutafuta fedha za kununulia vifaa vya kufundishia na kujifunzia wanafunzi.

Aidha, Mhe Rais Magufuli  amekipongeza chuo cha MUST kwa kuanzisha mafunzo ya ufundi mchundo na usadifu  na kuwaonya wanafunzi wa chuo hicho kuelekeza jitihada zao katika masomo badala ya masuala yasiyo ya msingi ikiwemo mahusiano ya kimapenzi

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Prof. Joyce Ndalichako amemshukuru Mhe Rais Magufuli kwa kutoa kipaumbele katika elimu na amebainisha kuwa pamoja na kujengwa maktaba hiyo Serikali imetoa sh. Milioni 482.6 kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa vya chuo hicho, imetoa sh milioni 702 kwa ajili ya kukarabati majengo ya chuo cha MUST kampasi ya Rukwa na sh. Milioni 483 kwa ajili ya kujenga mabweni ya wanafunzi 600 katika kampasi ya Rukwa.

Prof. Ndalichako ameongeza kuwa katika jitihada za kuboresha miundombinu ya vyuo vya elimu ya Juu Serikali imetoa shilingi bilioni 10.2 kwa ajili ya kujenga mabweni ya Chuo Kikuu cha Mzumbe  Mkoani Morogoro, ametoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kujenga jengo la Taaluma na Utawala na shilingi milioni 488.3 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya kampasi ya Tegeta  Dar-es-Salaam.                       Akisoma taarifa ya Chuo hicho Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Aloys Mvuma maktaba hiyo ina ghorofa 3 na uwezo wa kuchukua wasomaji 2500 kwa mara moja ikilinganishwa maktaba iliyopo hivi sasa ambayo inachukua wasomaji 150 

Matangazo

  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2021 Mkoa wa Mbeya. December 18, 2020
  • Matokeo ya Kidato cha Sita 2020 August 21, 2020
  • Matokeo ya Darasa la Saba 2020 November 21, 2020
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • Mkoa wa Mbeya Wajiwekea Malengo ya Upandaji miti

    January 13, 2021
  • Mbeya Yaja na Mkakati Mpya wa kupunguza Upungufu wa Vyumba Vya Madarasa

    December 09, 2020
  • Mbeya Waadhimisha Siku ya Uhuru kwa Kupanda Miti

    December 09, 2020
  • RC Aagiza Kuchunguza Upotevu wa 800M za Walimu

    December 04, 2020
  • Tazama Zaidi

Video

Viongozi watakiwa kuwa wasafi
Video

Viunganishi vya Haraka

  • Wasifu wa Mkoa wa Mbeya 2015
  • Mpango Mkakati wa Mkoa 2018-2023
  • Mbeya Regional GNP Report 2015
  • Barua Pepe za Watumishi
  • Mbeya kwa Namba
  • Utaratibu wa Uhamisho
  • Mpango Mkakati wa Kuendeleza Sekta za Kilimo 2020 - 2025
  • Fomu ya Ruhusa
  • Maoni na Malalamiko

Viunganishi Linganifu

  • Sekretarieti ya Ajira
  • Utumishi
  • Ikulu
  • Tovuti ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Ajira

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Uzunguni Road

    Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.

    Simu: 025 2503034

    Simu ya Mkononi: 255 784838650

    Barua pepe: ras@mbeya.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2019 Mbeya Region . All rights reserved.