The United Republic of Tanzania, President's Office Regional Administration and Local Goverment, Mbeya Region

Highlights and Resources

WATUMISHI WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

mkuu wa mkoa
WATUMISHI WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amewaambia watumishi wa hospitali ya Mkoa kutimiza wajibu wao katika kutoa huduma zenye viwango vya kuridhisha kwa wananhi.
Mhe. Makalla ameyasema hayo alipofanya kikao na watumishi wa umma kwa lengo la kujitambulisha na kusikiliza hoja mbalimbali za watumishi hao. Amewaasa madaktari kutoa huduma inayoridhisha kwa sababu kazi yao inahitaji uzalendo, huruma na maadili.
Aidha, ameagiza kutosikia malalamiko yoyote yanayohusu rushwa katika hospitali zote za Mkoa wa Mbeya. Mhe. Mkuu wa Mkoa ameahidi kuwa bega kwa bega na watumishi hao na hakuna wananchi watao wanyanyasa. Mtu yeyote atakayewafanyia fujo madaktari atashughulikiwa kisheria.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ameuagiza uongozi wa hospitali ya mkoa kuweka dirisha la wazee sehemu ya kupokelea wagonjwa ili kuwatambua mapema na kupata huduma kwa haraka.