The United Republic of Tanzania, President's Office Regional Administration and Local Goverment, Mbeya Region

Highlights and Resources

MKUU WA MKOA AWAPA SIKU SABA (7) TANROADS KUREKEBISHA BARABARA YA IGURUSI - LUHANGA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amempa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mbeya siku 7 kutembelea barabara ya Igurusi – Luhanga na kufanyia marekebisho kwenye sehemu korofi za barabara hiyo wakati wakisubiria fedha kwa ajili ya ujenzi kalavati.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kwanza aliyoifanya Mkoani Mbeya na kukutana na hangamoto ya ubovu wa barabara hiyo ya Igurusi – Luhanga. Mhe. Makalla amesema barabara hiyo ni muhimu kwa shughuli za kiuchumi na huduma za jamii hivyo ni muhimu ikafanyiwa ukarabati mapema.
Aidha, Mhe. Makalla amewaagiza TANROADS – Mbeya kuiweka barabara hiyo katika bajeti ya fedha wanazozipata kwa ajili ya matengenezo ya barabara. Pia ameahidi kurudi baada ya wiki moja kuangalia utekelezaji wa agizo hilo ulipofikia kwa sababu ubovu wa barabara hiyo unawaletea kero wananchi wanaoishi katika maaeneo hayo.