The United Republic of Tanzania, President's Office Regional Administration and Local Goverment, Mbeya Region

Highlights and Resources

MKUU WA MKOA WA MBEYA AFANYA UKAGUZI WA UKARABATI WA MABWENI YALIYOUNGUA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA

JENGO
Mkuu wa Mkoa Mhe. Makalla akikagua ukarabati wa moja ya bweni ShuLe ya Sekondari Iyunga

MKUU WA MKOA WA MBEYA AFANYA UKAGUZI WA UKARABATI WA MABWENI YALIYOUNGUA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla ametembelea shule ya sekondari Iyunga kuona maendeleo ya ukarabati wa mabweni yaliyoungua na moto na kuridhika na hatua zilizofikiwa na Halmashauri katika ukarabati huo.
Mhe. Makalla amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Mbeya kwa kuchukua uamuzi wa kuirudisha shule katika hali yake na kuwapongeza pia Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kutimiza wajibu wao wa kusimamia ukarabati wa mabweni hayo. Pia aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kuhangia vifaa vya ujenzi na fedha taslimu kwa shule hiyo.
Mkuu wa Mkoa aliagiza kutoanza ujenzi wa mabweni mapya badala yake ukarabati ufanyike kwa mabweni yote ya shule kwa kuangalia pia mfumo wa umeme na kukarabati nyumba za walimu.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Meya wa Jiji la Mbeya aliomba wadau mbalimbali wa elimu kujitokeza kwa wingi kuchangia ukarabati wa shule hiyo wakati Halmashauri imeshafanya sehemu yao. Meya wa Jiji alimshukuru pia Mkuu wa Mkoa kwa kutembelea shule hiyo
Aidha, Mkuu wa Mkoa ameomba ushirikiano na madiwa katika kufanya kazi na kuachana na masuala ya siasa kwani uchaguzi umeisha na imebaki kusukuma gurudumu la maendeleo kwa watu wa Mbeya. Pia ameahidi kutoa ushirikiano kutoka kwa madiwani bila kujali itikadi zao za vyama.
dARASA
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla akikagua ukarabati wa mabweni yaliyoungua shule ya Sekondari Iyunga.