The United Republic of Tanzania, President's Office Regional Administration and Local Goverment, Mbeya Region

Highlights and Resources

BODI YA BARABARA

Mkoa wa Mbeya/Songwe umepanga kutumia Shilingi Billioni 19.284 kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za barabara....

Mkoa wa Mbeya/Songwe umepanga kutumia Shilingi Billioni 19.284 kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za barabara katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo hadi sasa miradi yenye thamani ya shilingi billioni 11.437 sawa na asilimia 53.3 ya bajeti ya matengenezo imesainiwa.
Akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amesema kuwa utekelezaji wa kazi za barabara kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Halmashauri za Wilaya na Jiji la Mbeya kwa pamoja zimepanga kutumia shilingi billioni 8.580 ambapo hadi sasa Halmashauri hizo hazijapokea fedha za kazi hizo ingawa kazi hizo zimetangazwa na utaratibu wa kupata wakandarasi unaendelea.
Utekelezaji wa kazi za barabara kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Halmashauri za Wilaya na Jiji la Mbeya kwa pamoja na ilipanga kutumia fedha kiasi cha shilingi billioni 5.209. Fedha zilizopokelewa hadi sasa ni shillingi billioni 4.312.
Katika kusimamia miundombinu ya barabara Mkuu wa Mkoa ameagiza Wakuu wa Wilaya wote na Wakurugenzi wasitishe shughuli zote zinazoendelea katika hifadhi ya barabara na sheria ichukuemkondo wake kwa wote watakaoakiuka agizo hilo. Wakati huo huo Mhe. Makalla amekatazatabia ya wananchi kuchoma miundombinu ya barabara na kuleta uharibifu mkubwa.