The United Republic of Tanzania, President's Office Regional Administration and Local Goverment, Mbeya Region

Mbarali District

Wilaya ya Mbarali ni miongoni mwa Wilaya tisa na Halmashauri kumi zinazounda Mkoa wa Mbeya. Wilaya hii ilianzishwa mnamo tarehe 7 Julai, 2000 kwa mujibu wa vifungu vya 8 na 9 vya Sheria ya Serikali za mitaa ya mwaka 1982 na kupatiwa cheti kilichosainiwa tarehe 5 June, 2003.

 1. UTANGULIZI.

Wilaya ya Mbarali ni miongoni mwa Wilaya tisa na Halmashauri kumi zinazounda Mkoa wa Mbeya.  Wilaya hii ilianzishwa mnamo tarehe 7 Julai, 2000 kwa mujibu wa vifungu vya 8 na 9 vya Sheria ya Serikali za mitaa ya mwaka 1982 na kupatiwa cheti kilichosainiwa tarehe 5 June, 2003.

 1. MAHALI ILIPO NA MIPAKA YAKE.

Wilaya ya Mbarali ipo kati ya nyuzi 33.40 na 35.40 Longitudo kuelekea upande wa Mashariki, nyuzi 7.41 na 9.25 kusini ya Ikweta.  Upande  wa Kaskazini Mashariki, inapakana na Wilaya ya Iringa Vijijini, upande  wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Njombe, upande wa Kusini  kabisa inapakana na wilaya ya Mbeya na Kaskazini inapakana na Wilaya ya Chunya.

1.2. ENEO NA MATUMIZI YA ARDHI.

Wilaya ina jumla ya eneo la Kilometa za mraba 16,000 na mgawanyo wa matumizi ya ardhi ni kama inavyoonyesha kwenye jedwali No. 1.

 

JEDWALI I:

NA

MATUMIZI YA ARDHI

KM ZA

MRABA

HEKTA

ASILIMIA

YA UWIANO

1

Ardhi kwa  ajili ya kilimo

3,215

321,500

20.09

2

Eneo la wanyama pori

5,200

520,000

32.5

3

Hifadhi ya Misitu

172

17, 200

1.1

4

Eneo la makazi

6,078

607,800

38.0

5

Uwanda wa Tambarare, vilima, maeneo oevu na ufugaji

2,590

259,000

16.2

 

JUMLA

16,000

1,600,000

108

1.3. SURA YA NCHI

Wilaya ya Mbarali ipo uwanda wa chini wa tambarare wenye nyasi na sehemu kubwa ya Wilaya imepitiwa na Bonde la Ufa na maeneo yenye miinuko kwa upande wa Magharibi, ikiwa na mito mitatu ya kudumu.  Vile vile Wilaya ina chanzo kikuu cha maji ambacho ni Mto Ruaha Mkuu ambao baadaye huungana na mto Rufiji na kumwaga maji katika Bahari ya Hindi.

Wilaya imegawanyika katika kanda tatu za KIIKOLOJIA ambazo ni Uwanda wa Msangaji, Uwanda wa kati wa Usangu na Tambarare za Kusini mwa Usangu.

JEDWALI II:

NA

KANDA

MAHALI ILIPO

ALTITUDE (M)

UDONGO WA MVUA

SHUGHULI KUU ZA KIUCHUMI

1

Uwanda wa Msangaji (kanda ya Kaskazini)

 Ruaha National Park

1200-1800

 

 • Udongo wa mawe wenye rutuba ndogo
 • Mvua milimita 500-900 kwa Mwaka
 • Unyevunyevu miezi 3-5

Eneo lipo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA)

2

Uwanda wa kati wa tambarare  ya Usangu (Ukanda mkuu wa ufugaji)

 • Ruiwa
 • Ut/Usangu
 • Rujewa
 • Mapogoro
 • Sehemu ya kata ya Mawindi

1000-1400

Udongo mweusi na kichanga

Mvua mm 450-650 kwa mwaka

Unyevunyevu miezi 3-4

Kilimo cha mazao ya:

 • Mtama
 • Uwele
 • Ufugaji
 • Mahindi
 • Mpunga

3

Tambarare za Kusini  Usangu (ukanda wa kusini – kanda ya kilimo)

 • Ilongo
 • Rujewa
 • Chimala
 • Mapogoro
 • Igurusi
 • Ubaruku

750-1000

Mvua haba mm 360-750

Kilimo cha mazao ya:

 • Mahindi
 • Karanga
 • Pamba
 • Kilimo cha umwagiliaji Mpunga
 • Ufugaji

 

1.4. HALI YA HEWA NA UOTO

Wilaya ya Mbarali ipo katika latitude inayoanzia mita 1,000 – 1,800 juu ya usawa wa Bahari.  Wastani wa joto ni kati ya nyuzi 25c na 30c.  Wastani wa mvua hutofautiana kati ya milimita 300-940, hata hivyo kuna misimu miwili yaani msimu wa kiangazi ambao huanzia mwezi Mei – Novemba na msimu wa mvua ambao huanza Desemba – Aprili

Kwa ujumla Wilaya yote iko ndani ya uwanda wa Tambarare katika Bonde la Usangu ambalo lina uoto wa Asili aina ya Mipogoro.

Hali ya Mvua kwa Miaka Mitano iliyopita ni kama ifuatavyo:

NA

MWAKA

WASTANI WA MVUA (MM)

1

2005/2006

300.00

2

2006/2007

800.00

3

2007/2008

450.00

4

2008/2009

400.00

5

2009/2010

412.80

6

2010/2011

428.00

7

2011/2012

473.96

8

2012/2013

216.48

9

2013/2014

770

 

Hali hii ya upunguaji wa Mvua, inaathiri sana uzalishaji wa mazao ya kilimo hususani mpunga ambao ndio tegemeo kuu la mapato yetu ya ndani.

1.5. MUUNDO WA UTAWALA  NA MAKABILA.

Muundo  na utawala wa Wilaya ya Mbarali ni kama inavyoonyesha kwenye jedwali.

JEDWALI III

TARAFA

MAJIMBO YA UCHAGUZI

KATA

VIJIJI

VITO NGOJI

KAYA

WAH. MADIWANI

KUCHAGU

LIWA

KUTEULIWA

JML

2

1

20

103

713

69,888

 

 

 

1.6 MAKABILA

Makabila makuu yaliyopo Wilayani Mbarali ni Wasangu, Wahehe, Wakinga, Wabena na Wanyakyusa.  Vile vile yapo makundi madogo ya makabila wakiwemo Wasukuma, Wanji, Wabarbeig na Wagogo.

Makundi mengi ya makabila haya ni wakulima na wafugaji ambao walihamia bonde la Usangu kutoka Mikoa ya Arusha, Mwanza, Shinyanga, Singida na Dodoma.

1.7. IDADI YA WATU

Kufuatia sensa ya kitaifa ya idadi ya watu ya mwaka 2012, Wilaya ya Mbarali sasa ina jumla ya watu 300,517 ambao kati yao 145,867ni wanaume na 154,650 ni wanawake ikiwa na ukuaji wa 2.8%.

1.8. IDADI YA WATUMISHI.

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ina jumla ya watumishi 2,527. Mahitaji ni watumishi 2,971 hivyo kuna upungufu wa watumishi wapatao 1,012 kama jedwali linavyoonyesha hapa chini;

JEDWALI IV

Na

IDARA/KITENGO

IKAMA ILIYOIDHINI SHWA

WATUMISHI WALIOPO

UPU NGUFU

ZIADA

1

Utawala na Utumishi

144

130

14

-

2

Fedha na Biashara

22

19

3

-

3

Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji

6

5

1

-

4

Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika

134

83

51

 

-

5

Mifugo na Uvuvi

128

48

80

-

6

Elimu ya Msingi

1648

1193

455

-

7

Elimu ya Sekondari

495

434

61

-

8

Maji

13

7

6

-

9

Ujenzi

30

21

9

-

10

Afya

688

365

323

-

11

Ardhi na Maliasili

26

21

5

-

12

Maendeleo ya Jamii

27

23

4

-

 

JUMLA

2,971

2,527

1,012

-

1.9: MWENENDO WA MAPATO NDANI YA HALMASHAURI

Halmashauri imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo na ustawi wa jamii kupitia Mapato yake ya Ndani yanayotokana na vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushuru wa mazao, ushuru kutokana na huduma mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri. Mwenendo wa mapato ya ndani ya Halmashauri ni kama ifuatavyo:-

JEDWALI V

NA

MWAKA

MAKISIO

MAPATO

ASILIMIA (%)

1

2007/2008

319,882,060

487,449,295

152

2

2010/2011

478,894,538

666,742,372

139

3

2009/2010

       721,124,000

    639,527,000

88.7

4

2010/2011

       728,757,700

    621,890,570

85.3

5

2011/2012

773,027,000

934,388,639

121

6

2012/2013

1,348,748,000

915,496,546

67.9

7

2013/2014

1,602,798,000

1,396,807,050.55

87.1

8

2014/2015

2,672,063,706

1,921,741,556.72

72

2.0: SHUGHULI ZA KIUCHUMI.

Uchumi wa Wilaya ya Mbarali unategemea kwa kiwango kikubwa uzalishaji wa mali vijijini hasa sekta ya Kilimo, wastani wa asilimia 83  ya wakazi Wilaya ya Mbarali hujishughulisha na kilimo, shughuli zingine za kiuchumi ni pamoja na ufugaji, uvuvi na biashara ndogondogo; kwa ujumla wake pato la mkazi wa Mbarali ni shilingi 376,500/= kwa mwaka.                                       

2.1 KILIMO

Asilimia 83 ya wakazi wa Wilaya ya Mbarali hujishughulisha na kilimo na ufugaji.  Mazao muhimu ya chakula ni pamoja na Mpunga, Mahindi, Viazi vitamu, Mihogo, Maharage na Mtama.  Hata hivyo mpunga huzalishwa kama zao la chakula na biashara.  Mazao ya biashara ni Alizeti, Karanga na Mazao ya bustani.

Kutokana na hali ya hewa isiyotabirika na kupungua kwa mvua, Halmashauri imekuwa inawekeza katika Kilimo cha umwagiliaji.

Mpaka sasa, Wilaya ya Mbarali ina jumla ya skimu za umwagiliaji 80 zenye jumla ya hekta 78,953. Kati ya hizo skimu 34 zimeboreshwa zenye jumla ya eneo linalofaa kulimwa hekta 41,724 lakini zinazolimwa ni 23,519. Aidha skimu 46 hazijaboreshwa zengye jumla ya eneo linalofaa kulimwa hekta 37,229 lakini zinazolimwa ni 20,989.

Juhudi zinaendelea za kuboresha miundombinu ya skimu za kilimo cha umwagiliaji, kuwajengea uwezo wakulima ili waweze kuzalisha kwa tija zaidi, Ujenzi wa miundombinu ya masoko (maghala na viwanda vya usindikaji) na kuboresha barabara za vijijini  zipitike kwa urahisi.

2.2. MALIASILI

Wilaya ina utajiri wa maliasili mbalimbali ikiwa ni pamoja na misitu, wanyamapori, madini, ufugaji nyuki, samaki na sehemu ya hifadhi ya Taifa Ruaha, vilevile pori la akiba la Usangu.

3.0 HUDUMA ZA KIJAMII NA FURSA ZILIZOPO

3.1 ELIMU

Wilaya ina shule/vyuo kama ifuatavyo:

Jedwali vII

NA

AINA YA SHULE

SERIKALI

BINAFSI

TAASISI

JUMLA

1

Shule za awali

100

-

2

102

2

Shule za msingi

103

2

-

105

3

Shule za sekondari

16

1

6

23

4

Vituo vya EWW

5

-

-

5

5

Vituo vya MUKEJA

12

-

-

12

 

 • Idadi ya wanafunzi wa shule za msingi                    51,999
 • Idadi ya wanafunzi wa shule za sekondari               9,580
 • Idadi ya walimu shule za msingi                                1,193
 • Uwiano wa walimu na wanafunzi                              1:44

Kwa Mwaka wa masomo 2013 kiwango cha  ufaulu kwa Elimu ya Msingi ni 70.0%

Wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kuingia Sekondari ni 4143. Wanafunzi hao wote walipata nafasi ya kujiunga na Kidato cha Kwanza.

Kiwango cha ufaulu Kwa Elimu ya Sekondari ni; Kidato cha pili 94.87% na Kidato cha nne 71.23% (83.23%).

Aidha kwa upande wa Walimu hali halisi iko kama ifuatavyo:

JEDWALI VII

Sekta

Idadi ya Walimu

Asilimia ya Upungufu

Wanaohitajika

Waliopo

Upungufu

Elimu ya Msingi

1299

1193

106

8

Elimu ya Sekondari

597

506

91

15

3.2 AFYA

Wilaya ina vituo vya kutolea huduma ya afya kama ifuatavyo:

JEDWALI VIII

NA

VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA

SERIKALI

BINAFSI

TAASISI

JUMLA

1

Hospitali

1

-

1

2

2

Kituo cha afya

5

-

1

6

3

Zahanati

34

2

4

40

Kwa upande wa Rasilimali watu katika Idara ya Afya, hali iko kama ifuatavyo:

Shule

Idadi ya Watumishi

Asilimia ya Upungufu

Wanaohitajika

Waliopo

Upungufu

Hospitali ya Wilaya

211

164

47

22.3

Afya Kinga

26

11

15

57.7

Vituo vya Afya 5

195

87

108

55.4

Zahanati 34

510

185

325

63.7

JUMLA

942

447

495

52.5

3.3 MAJI

Wilaya ya Mbarali ina mtiririko wa mito inayoanzia safu ya milima ya kipengele na uproot, vyanzo hivi vimekuwa mtego wa maji ya bomba kwa vijiji 76 kati ya 93 vya Wilaya nzima.

JEDWALI VI:

NA

VYANZO VYA MAJI

IDADI

IDADI YA VIJIJI VINAVYONUFAIKA       NA HUDUMA

IDADI YA  WATU      WANAONUFAIKA NA HUDUMA

1

Miradi ya kutegwa (gravity scheme)

10

52

160,848

2

Visima virefu (Borehole)

36

15

36,104

3

Visima vifupi (Borehole)

47

10

13,533

 

JUMLA

93

77

210,485

 

 

 

 

 

 

 

 

 

3.4 BARABARA

Wilaya  ina mtandao  wa barabara zilizoanzishwa zenye urefu wa km 1,308.2 ambazo kati ya hizo, barabara zenye urefu wa km 305.5 zinahudumiwa na meneja wa TANROADS na km 1002.7 zinahudumiwa na Halmashauri. Barabara zinazohudumiwa na Halmashauri zimegawanyika kama ifuatavyo;

JEDWALI VII

NA

AINA YA BARABARA

UREFU

1

Barabara ya changarawe

Km 216.15

2

Barabara ya changarawe/udongo

Km 786.55

Aidha kuna km 555.95 ambazo hazijaandikishwa na zinahudumiwa na Halmashauri, baada ya kupitishwa na Baraza la Madiwani mwaka 1998 ili kuweza kufikia maeneo ya uzalishaji na utawala, ili kuboresha ujenzi wa uchumi katika Wilaya.  Kati ya km 555.95 km 86.7 ni za changarawe na km 469.25 ni za udongo.

3.5 VYAMA VYA USHIRIKA

Vyama vya ushirika ni vyombo muhimu katika kumkomboa mwananchi kutokana na umaskini.  Hali ya vyama vya ushirika katika wilaya ya Mbarali ni kama ifuatavyo:

JEDWALI VIII

NA

 

AINA YA USHIRIKA

WANACHAMA

MTAJI

Tshs.’000,000

MIKOPO Tshs.’000’000

IDADI

MOJA

MOJA

VIKUNDI

JUMLA

HISA

AMANA

AKIBA

TOLE

WA

REJESHA

1

Ushirika wa Akiba na Mikopo

 

24

7,191

209

7,400

1282.5

430.9

2028.8

23.404.7

14,347.3

2

Ushirika wa usafirishaji wa mazao ya kilimo

3

86

-

86

12.4

-

-

-

-

3

Ushirika wa kilimo na masoko

8

4,168

14

4,182

316.6

-

-

-

-

4

Ushirika wa wafugaji

1

18

-

18

0.64

-

-

-

-

5

Ushirika wa kilimo na umwagiliaji

9

2,808

8

2,816

12.3

-

-

-

-

6

Ushirika wa biashara ya samaki

4

170

0

170

13.85

-

-

-

-

7

Wabeba mifugo

1

19

 

 

1

 

 

 

 

 

JUMLA

50

15397

2028

15705

2593

378

2581

15801

12318

3.6. VIKUNDI VYA KIUCHUMI VYA WANAWAKE NA VIJANA

Katika kuhakikisha umaskini unapungua kwa jamii wa wilaya ya Mbarali huduma ya mikopo kwa vikundi vya kiuchumi vya wanawake na vijana imekuwa ikitolewa tangu mwaka 1998 hadi 2013 kama inavyoonyesha:-      

JEDWALI IX:

MWAKA

VIKUNDI

MKOPO TOLEWA

RIBA (10%)

MKOPO + RIBA

MAREJESHO

BAKI

% YA MAREJESHO

Bakaa 2006

82

70,993,000

9,122,800

80,115,800

79,626,554

1,233,454

99.39

2007

17

18,000,000

1,800,000

19,800,000

19,590,000

210,000

98.93

2008

14

15,200,000

1,520,000

16,720,000

16,180,000

540,000

96.77

2009

4

4,000,000

400,000

4,400,000

4,400,000

0

100

2010

12

10,350,000

1,755,000

11,385,000

11,385,000

0

100

2013

3

6,000,000

600,000

6,600,000

4,600,000

2,000,000

69.69

JUMLA

32

124,543,000

15,197,800

139,020,800

135,781,554

3.983,454

97.66

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

MIKOPO YA WANAWAKE CHINI YA  MFUKO WA WDF

JEDWALI X:

MIKOPO YA VIKUNDI VYA VIJANA KUTOKA SERIKALI KUU NA H/WILAYA

MWAKA

KIKUNDI

MKOPO TOLEWA

RIBA (15%)

MKOPO + RIBA

MAREJESHO

BAKI

%

2006

7

3,000,000

450,000

3,450,000

3,450,000

-

100

2007

18

6,900,000

1,035,000

7,935,000

7,497,000

438,000

94.48

2008

4

2,000,000

300,000

2,300,000

1,885,000

415,000

81.96

2009

2

10,000,000

500,000

10,500,000

10,475,500

  24,500

9977

JUMLA

25

21,900,000

2,285,000

24,185,000

23,307,500

24,500